Imenakiliwa kutoka kwa Imam Swadiq(amani ziwe juu yake) akisema ya kuwa: ((Raas Al-sanat laylat Qadr, yuktab fiiha ma yakunu min sanat ila sanatin )) Mwanzo wa mwaka, ni usiku wa Qadr, kwani katika usiku huo kila ambacho kitatokea katika mwaka huu mpaka mwaka mwengine, basi huwa kinaandikwa.Vile vile imekuja riwaya hii kutoka kwa Imam Baqir(amani ziwe juu yake): ((Man ahya laylatul Qadr, ghufira lahu dhunubahu walaw kaanat adad nujum Al_Samaai wa mithaqiil Al_Jibaal wa makaail Al_Bahr)) Yeyote yule ambaye ataupitisha kwa ibada usiku wa Qadr, basi atasamehewa madhambi yake hata kama ni makubwa mfano wa idadi ya nyota zilizoko mawinguni na uzito wa milima na maji ya bahari zote.Bilashaka ni lazima kuwa waangalifu kwani malipo haya na thawabu hizi ni kwa ajili ya wale watu ambao wanatimiza masharti ya kukubaliwa ibada zao na kwa kutenda dhambi za makusudi au kupinga amri za Mwenyezi Mungu basi mambo haya yanaweza kuharibu malipo yao.Imam Mussa bin Jafar(amani ziwe juu yake) anasema: ((Mani Gh_tasal laylatul Qadr wa ahyaaha ila tulughil fajri, Khurija min dhunuubih)) Mtu yeyote ambaye ataoga katika usiku wa Qadr na akasimama kwa ajili ya ibada mpaka mapambazuko ya alfajiri, basi ataondokana na madhambi yake. Mtu ambaye anashukiwa na malaika wote wa Mwenyezi Mungu katika usiku wa Qadr, ni mwenyewe mtukufu muhimili wa ulimwengu na tegemeo la viumbe, mtukufu Baqiyat Allah (roho zetu ni fidia kwake). Inapendeza kwa wapenzi wa mtukufu huyo kwa heshima na unyenyekevu katika muda wote hasa hasa katika usiku wa mwezi kumi na tisa, ishirini na moja, ishirini na tatu wa Ramadhani, kwa ajili ya kudhihiri kwa mtukufu huyo kusoma dua na kurejea mara kwa mara dua tukufu ya Imam Zamani (( Ewe Mwenyezi Mungu mfanye kiongozi …...)) hasa katika usiku wa mwezi ishirini na tatu usighafilike, na kufanya tawasul kwa Imam huyo mpaka upate baraka na fadhila za usiku wa Qadr.
26 Julai 2013 - 19:30
Msimbo wa Habari: 445700
Usiku wa Qadr ni usiku wenye fadhila nyingi sana kuliko usiku wa mwaka mzima, ambapo kutokana na riwaya mambo yatakayokuwepo ulimwenguni huwa yanapangwa katika usiku huo. Na kwa upambanuzi wa Imam kila zama hufika usiku huo.